Sunday, 8 November 2015

Lyrics to Zaburi moja by Fred Obare



Katika njia zako zote mkiri Bwana Yesu
Naye atayanyosha wewe mapito yako

Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki eh
Wala kusimama katika njia ya wakosaji
Pia hakuketi barazani pa wenye mizaha eeh

Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki eh
Wala kusimama katika njia ya wakosaji
Tena hakuketi barazani pa wenye mizaha eeh

Kwani sheria ya Bwana ndiyo impendezayo
Yeye huitafakari mchana na usiku eh

Naye atakua kama mti uliopandwa kando kando ya vijito
Vijito vya maji uzaao matunda yake kwa majira yake
Wala jani lake yeye halinyauki
Na kila alitendalo yeye litafanikiwa eeh

Naye atakua kama mti uliopandwa kando kando ya vijito
Vijito vya maji uzaao matunda yake kwa majira yake
Wala jani lake yeye halinyauki
Na kila alitendalo yeye litafanikiwa eeh

Sivyo walivyo wale wasio haki eh
Wao ni kama makabi eeh
Yapeperushwayo na upepo
Na kwa hivyo wale wasio haki eh
Hawatasimama hukumuni eh
Wala katika mkusanyiko wa wenye haki eeh

Sivyo walivyo wale wasio haki eh
Wao ni kama makabi eeh
Yapeperushwayo na upepo
Na kwa hivyo wale wasio haki eh
Hawatasimama hukumuni eh
Wala katika mkusanyiko wa wenye haki eeh


Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki
Kwani njia ya wasio haki litapotea
Katika njia zako zote mkiri yeye
Naye atayanyosha wewe mapito yako

Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki
Kwani njia ya wasio haki litapotea
Katika njia zako zote mkiri yeye
Naye atayanyosha wewe mapito yako


No comments:

Post a Comment