Wednesday, 22 October 2014

Usichoke by Ayzoh Levite





wimbo huu ni wako
baba yangu, mama yangu
kwako dada kijana
eiya nasema

Imepita miaka huku wangoja matokeo
Unajiuliza itakuwa vipi ei
Uliowadhamini wamekuweka kando
Eti kwa sababu hauna chako wewe
Usikate tamaa usiangalie nyuma
Mtazamie Yesu aliye na jawabu lako wewe

Usichoke endelea kungoja tu
Usichoke subiri kidogo mambo yatajipa wewe
Usichoke endelea kungoja tu
Usichoke Mola hachelewi tena
Hana chuki yeye

Bwanangu naomba unitegee sikio lako
Ninayokueleza yasije yakatoka moyoni mwako
Kama yawezekana yaandike vitangani mwako
Ama uyachore kwa wino yasije yakafutika
Huyu Bwana hachelewi wala hananga pupa
Kwa wakati ufaao yeye huja na
Kutekeleza mapenzi yake kwako


Usichoke endelea kungoja tu
Usichoke subiri kidogo mambo yatajipa wewe
Usichoke endelea kungoja tu
Usichoke Mola hachelewi tena
Hana chuki yeye


Usichoke mumy usichoke baba
Usichoke dada
Ndugu yangu usichoke kamwe
Usichoke usichoke Usichoke
Endelea kungoja Bwana wewe

No comments:

Post a Comment