Ayeyeyeye mganga wa kweli eh
Njoni nyote niwaonyeshe
Mimi nimemwona
Mganga (nimemwona eh) Mganga (nimemwona)
Mganga wa waganga ni YESU
Mimi nimemwona
Mganga (nimemwona eh) Mganga (nimemwona)
Mganga wa waganga ni YESU
Nasema nimemwona Mganga wa waganga
Anayeinamiwa na waganga wote
Hata na wachawi pia
Wanaleta madawa yao, hata na hirizi
Na wanatangaza maovu yote walotendea wanadamu
Huyu Mganga kazaliwa Bethlehemu
Kalelewa Nazareti
La ajabu ni mwana wa bikira
Nimemwona
Mganga (nimemwona) Mganga (nimeona Mganga)
Mganga wa waganga ni YESU
Mimi Ye nimemwona
Mganga (nimeona Mganga) Mganga (Hai Mganga YESU)
Mganga wa waganga ni YESU
Jina la huyu Mganaga kwa kweli lanishangaza
Kwa maana lina nguvu nyingi kama mganga mwenyewe
Lilipotajwa na Petero Tabitha kafufuka
Kiwete njiani akatembea kwa ajili ya hilo jina
Paulo na Sila wakasifu kwa hilo jina
Milango ya gereza ikafunguka kwa jina la Mganga YESU
Nimemwona
Mganga (nimemwona) Mganga (Hai nimemwona)
Mganga wa waganga ni YESU
Mimi ndio nimemwona
Mganga (nimeona Mganga) Mganga (Hai Mganga YESU)
Mganga wa waganga ni YESU
Nguo za huyu Mganga hata nazo zina nguvu eh!
Mama aliyevuja damu alipenya katikati ya umati
Kaguza upinde wa nguo damu ikakatika
YESU akamwambia imani yako ndiyo imekuponya
Baada ya kusulubiwa heh! Nguo za huyu mganga
Hazingepasuliwa kwa bei yake zikapigiwa kura
Nimemwona
Heh! Nimeona Mganga
Amebadili maisha yangu
Ukiomba kwa jina lake majabu yanatendeka
Mganga wa kweli
Haiyeyeyye ah
Mganga (Nao wakimbia kwa waganga) Mganga
(Njoni Muone Mganga)
Mganga wa waganga ni YESU
Mganga Yesu
Mganga Mganga
(hakuitishi chochote)
Mganga wa waganga ni YESU
(Aliye mganga wangu)
Mganga Mganga
(Ukimwamini anakwambia)
Mganga wa waganga ni YESU
(Aliye Mganga wangu)
Mganga Mganga
(Imani yakuponya)
Mganga wa waganga ni YESU
(Ukimwamini akwambia)
Mganga Mganga
(Enda usitende dhambi)
Mganga wa waganga ni YESU
(Aliye mganga wangu)
Mganga Mganga
(Omba kwa jina lake aliye Mganga wangu)
Mganga wa waganga ni YESU
(Ukiomba kwa jina lake biashara zina nawiri)
Mganga Mganga
(Haya akuongeza imani)
Mganga wa waganga ni YESU