Thursday, 18 July 2013

Naomba Lyrics , sung by Adawnage Band

Naomba Baba, minaomba, mikono nimeinua
Nishike Baba, unifiche eh, mikononi mwako
Nionyeshe Baba wema wako, unifanye chombo chako,
Ninaomba, naomba, Baba mie naomba

Sikudhani mimi, nimekupa weh huzuni kiasi hicho,
Dhambi nyingi, maombi hayatoki nisamehe Baba
Uchovu na uvivu umenijaza moyoni sina amani,
Naomba unipe raha, msamaha, naomba uwashe taa

Popote niendapo chochote nifanyacho sasa nifungue macho,
Nipate kuona na kuhisi, nipate upako wako

Naomba Baba, minaomba, mikono nimeinua
Nishike Baba, unifiche eh, mikononi mwako
Nionyeshe Baba wema wako, unifanye chombo chako,
Ninaomba, naomba, Baba mie naomba

Sikudhani mimi, nikiteleza ah, nakusulubu tena
Uchungu mingi machozi yakutoka weh, nisamehe Baba,
Nizibie ufa nisijenge ukuta Bwana, umetukuka
Naomba unipe raha,msamaha, naomba uwashe taa

Popote niendapo chochote nifanyacho sasa nifungue macho,
Nipate kuona na kuhisi, nipate upako wako

Naomba Baba, minaomba, mikono nimeinua
Nishike Baba, unifiche eh, mikononi mwako
Nionyeshe Baba wema wako, unifanye chombo chako,
Ninaomba, naomba, Baba mie naomba

Eeeee iii eeeh, Baba mie naomba

No comments:

Post a Comment